• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wahamiaji 164 haramu wahamishwa kwa hiari Niger kutoka Libya

  (GMT+08:00) 2019-01-11 09:25:58

  Shirika la Kimataifa la Uhamiaji IOM limesema, wahamiaji 164 haramu kutoka Niger wamerudishwa nyumbani kwa hiari kutoka Libya.

  Shirika hilo limesema wahamiaji 164 kutoka Niger wameweza kurudi nyumbani salama kupitia uwanja wa ndege wa Misurata. Vikundi vya shirika hilo vitaendelea kutoa msaada unaohitajika kwa wahamiaji waliosalia nchini Libya chini ya uungaji mkono wa Mfuko wa Umoja wa Ulaya.

  Mradi wa kuwarejesha kwa hiari wahamiaji hao unatekelezwa na IOM kwa lengo la kupanga kurejeshwa kwa wahamiaji haramu waliosalia nchini Libya kwenye nchi zao za asili.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako