• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Manara awaita mashabii Simba kuujaza uwanja kwa Mchina

  (GMT+08:00) 2019-01-11 09:30:08

  Afisa habari wa klabu ya Simba ya Tanzania amewaita mashabiki wa klabu hiyo kufika kwa wingi kwenye dimba la uwanja wa taifa kesho Jumamosi kuishangilia timu yao itakapomenyana na JS Saoura ya Algeria hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa Afrika.

  Mapema wiki hii, Simba ilitangaza viingilio vya mechi hiyo ambapo kima cha juu ni shilingi laki moja za kitanzania, wakati VIP B ni shilingi elfu kumi na kwa viti vya mzunguko ambako mashabiki wengi hupenda kukaa kiingilio ni shilini elfu tano za kitanzania.

  Mgeni rasmi katika pambano hilo la kukata na shoka ni Naibu Spika wa Bunge la Jmahuri ya Muungano wa Tanzania, Tulia Atson.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako