• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Walinzi wawili wa Gor Mahia wapigwa stop na CAF

  (GMT+08:00) 2019-01-11 09:30:27

  Mwamba wa Kenya Gor Mahia itawakosa mabeki muhimu Haron Shakava na Joash Onyango katika mchezo dhidi ya New Star ya Cameroon mchezo utakaopigwa jijini Nairobi Jumapili hii.

  Gor itaikaribisha New Star katika mechi ya mtoano wa kufuzu hatua ya makundi ya kombe la shirikisho barani Afrika.

  Shakava na Onyango wameadhibiwa na Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) kwa utovu wa nidhamu katika mechi ya marudiano dhidi ya Lobi Stars ya Nigeria kwenye Klabu Bingwa Afrika mnamo Desemba 22 mwaka jana mjini Enugu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako