• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • KIKAPU: Lebron kuendelea kukaa nje kutokana na majeraha

  (GMT+08:00) 2019-01-11 09:30:58

  Klabu ya mpira wa kikapu ya Los Angeles Lakers inayoshiriki ligi kuu ya kikapu nchini Marekani ya NBA, imetoa taarifa ya maendeleo ya mchezaji wao wa kutegemewa Lebron James aliyeumia na kutoruhusiwa kurudi uwanjani kwa muda mfupi.

  Daktari anayemhudumia Labron ameweka bayana kuwa mchezaji huyo ataendelea kuwa nje ya uwanja na kukosa mechi tatu zaidi zinazofuata kutokana na kuumia mguu wa kushoto mwishoni mwa mwaka jana.

  Lakers wanatarajia kukutana na Utah Jazz katika mchezo wa ugenini na kurejea katika uwanja wao wa nyumbani na kukutana na Cleveland Cavaliers pamoja na Chicago Bulls.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako