• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Idadi ya matukio ya usalama katika eneo la Sahel na Afrika magharibi yaongezeka

  (GMT+08:00) 2019-01-11 18:44:01

  Mjumbe wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia mambo ya Afrika magharibi na eneo la Sahel Bw. Mohamed Ibn Chambas ametahadharisha kuwa, idadi ya mashambulizi yanayofanywa na makundi yenye msimamo mkali katika eneo hilo imeongezeka kwa kasi, wakati nchi nyingi za eneo hilo zinatarajia kufanya uchaguzi mkuu.

  Bw. Chambas amesema, katika miezi kadhaa iliyopita, mashambulizi ya kundi la Boko Haram dhidi ya vituo vya kijeshi yameongeza kwa kasi. Pia kutokana na ongezeko la idadi ya matukio ya usalama, majimbo 7 kati ya majimbo 13 ya Burkina Faso yametangaza hali ya hatari.

  Bw. Chambas pia amesema, tishio hilo la usalama ni kutokana na ongezeko la idadi ya watu, ukosefu wa ajira kwa vijana na kufutwa kwa misaada ya maisha kutoka serikalini.

  Habari nyingine zinasema, naibu balozi wa China katika Umoja wa Mataifa Bw. Wu Haitao amesema, jumuiya ya kimataifa inapaswa kuongeza ushirikiano ili kukabiliana na changamoto ya usalama katika eneo hilo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako