• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yazitaka pande husika zitekeleze makubaliano ya amani ya Yemen

  (GMT+08:00) 2019-01-11 18:57:34

  Balozi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Bw. Ma Zhaoxu amezitaka pande husika kutekeleza kihalisi makubaliano yaliyofikiwa kwenye mazungumzo ya amani ya Yemen.

  Akizungumza katika mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa kuhusu suala la Yemen, Balozi Ma amezitaka pande hizo kutekeleza makubaliano ya kusimamisha vita mjini Hodeidah, kuhimiza mchakato wa kudumu na wenye ufanisi wa mazungumzo na kuendelea kutoa umuhimu wa usuluhishi wa Umoja wa Mataifa. Amesema kazi ya kutekeleza makubaliano ya kubadilishana mateka na kutatua suala la Taiz imeanza, na inaendelea vizuri. Pia balozi huyo amesema changamoto kadhaa bado zipo, ikiwemo mapambano yanatokea huko Hodeidah na hali mbaya ya kibinadamu nchini Yemen. Ametoa wito kwa pande husika kutekeleza makubaliano ya mazungumzo ya amani na maazimio husika ya Baraza la Usalama.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako