• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Iran kurusha satalaiti mbili ndani ya wiki kadhaa

  (GMT+08:00) 2019-01-11 19:00:19

  Rais Hassan Rouhani wa Iran leo amesema, nchi hiyo itarusha satalaiti mbili mpya katika wiki kadhaa zijazo.

  Rais Rouhani aliyasema hayo kwenye kumbukumbu ya miaka miwili tangu aliyekuwa rais wa Iran Akbar Hashimi Rafsanjani kufariki dunia. Amesema, maendeleo ya mfumo wa kujilinda na maendeleo ya sayansi na teknolojia ni mchango wa hayati rais huyo.

  Rais Rouhani hakutaja aina ya satalaiti zitakazorushwa, matumizi yake, na aina ya roketi zilizozirusha, lakini kwa mujibu wa wizara ya habari na teknolojia, Iran imekamilisha jaribio la urushaji wa satalaiti mpya zilizotengenezwa nchini humo, ambazo zitatumika kwenye sekta za kilimo, uhifadhi wa mazingira na usimamizi wa rasilimali ya maji.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako