• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mawaziri wa mambo ya nje wa China na Sierra Leone wakutana mjini Beijing

    (GMT+08:00) 2019-01-11 19:15:06

    Mjumbe wa taifa wa China ambaye pia ni waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi leo hapa Beijing amekutana na mwenzake wa Sierra Leone Dr. Alie Kabba ambaye yuko ziarani nchini China.

    Bw. Wang Yi amesema, China inapenda kushirikiana na Sierra Leone kuweka mpango halisi wa utekelezaji wa matokeo yaliyofikiwa kwenye mkutano wa kilele wa FOCAC uliofanyika Beijing. Pia pande mbili zinapaswa kuimarisha utaratibu wa kimkakati katika mambo ya kimataifa, kuhimiza uratibu wa kimataifa uendelezwe kwa mwelekeo wa haki na usahihi zaidi.

    Kwa upande wake Dr. Kabba, amesema Sierra Leone inapenda kuiga uzoefu wa China wa utawala wa taifa na kuzidisha ushirikiano wa kunufaishana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako