• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Watu wawili wauawa katika vurugu nchini DRC baada ya matokeo ya uchaguzi kutangazwa

  (GMT+08:00) 2019-01-11 19:15:32

  Watu wawili wameuawa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wakati vurugu zilipotokea baada ya mgombea wa upinzani Felix Tshisekedi kutangazwa mshindi katika uchaguzi wa rais.

  Katika mji wa magharibi wa Kikwit, watu wawili waliuawa kwa kupigwa risasi na wengine kadhaa kujeruhiwa wakati wa maandamano dhidi ya matokeo ya uchaguzi yaliyotangazwa na tume ya uchaguzi ya nchi hiyo jana asubuhi. Waandamanaji pia walichoma moto jengo lenye ofisi za polisi huku mabasi manne ya usafiri wa umma pia yakichomwa moto.

  Katika miji ya Kisangani na Goma, polisi waliwatawanya wafuasi wa Martin Fayulu, ambaye amechukua nafasi ya pili kwa wingi wa kura akimfuata Tshisekedi.

  Kwa mujibu wa matokeo ya muda yaliyotolewa na tume ya uchaguzi, Tshisekedi, ambaye ni mgombea kutoka chama cha UDPS amepata zaidi ya kura milioni 7 nchini humo. Hata hivyo, majimbo matatu hayajapiga kura kutokana na sababu za kiusalama.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako