• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya: Familia ya Kenyatta yanunua Benki ya Jamii Bora

  (GMT+08:00) 2019-01-11 20:13:07
  Commercial Bank of Africa (CBA) inayomilikiwa kwa kiasi kikubwa na jamii ya Kenyatta, imetoa shilingi bilioni 1.4 kuinunua Jamii Bora Bank. Hii itaongeze kwenye idadi, biashara tajika nchini Kenya zinazomilikiwa na familia ya aliyekuwa rais wa kwanza wa Kenya Hayati Mzee Jomo Kenyatta. Kando na biashara za benki, familia ya Kenyatta inamiliki kampuni ya kuzalisha maziwa ya brookside, kampuni za kuuza nyumba, viwanda na nyinginezo.

  Ununuzi wa Jamii Bora Bank unajiri wiki chache baada ya Commercial Bank of Africa (CBA) kutangaza kuwa itakuwa ikiendesha shughuli za benki ya NIC. Kujumuishwa kwa CBA, NIC na Jamii Bora Bank kutaiweka katika nafasi ya tatu kwa ukubwa kwenye sekta ya benki nchini Kenya baada ya benki za KCB na Equity.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako