• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya: Rais Uhuru Kenyatta aamrisha bei mpya ya mahindi

  (GMT+08:00) 2019-01-11 20:13:26
  Rais Uhuru Kenyatta ameagiza bodi ya nafaka na mazao nchini Kenya (NCPB) kununua mahindi kutoka kwa wakulima kwa shilingi 2,500 kwa kila gunia la kilo 90. Bei hii mpya ambayo imeongezwa kwa shilingi 200, imetangazwa huku kukiwa na malalamishi kutoka kwa wakulima wa mahindi kuhusiana na hasara wanayopata kwa kuuza mahindi kwa bei ya chini sana.

  Kando na hili, serikali pia imepunguza idadi ya magunia ya mahindi yatakayonunuliwa kutoka magunia milioni 2.5 hadi magunia milioni mbili. Wakulima wanaomba serikali kununua mahindi kwa shilingi 3,200 kwa kila gunia la mahindi la kilo tisini.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako