• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania-NSSF kuwajumuisha wavuvi kwenye mpango wa mafao

  (GMT+08:00) 2019-01-11 20:13:43

  Mfuko wa Taifa wa Jamii (NSSF) ,umedhamiria kuwafikia wavuvi katika maeneno mbalimbali nchini Tanzania,ili waweze kufaidika na mafao ambayo yamekuwa yakitolewa.

  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Mfuko huo,Lulu Mengele aliyasema hayo jana jijini Dodoma wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu mfuko huo.

  Alisema kuwa lengo la mfuko huo ni kuhakikisha unawafikia watu wa makundi mbalimbali katika jamii zote ili waweze kunufaika na huduma ambazo wamekuwa wakizitoa zitakazowasaidia kuwakinga katika majanga mbalimbali.

  Aidha Mengele alisema kuwa sababu za kuanzisha mpango wa hifadhi ya jamii kwa wavuvi umekuja baada ya kubaini kuwa wavuvi wana sifa za kujiunga na mpango huo,lakini walikuwa hawajui faida zake na hivyo kukosa mambo muhimu wao na familia zao.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako