• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanznaia: Ndege nyingine mpya yawasili Tanzania

  (GMT+08:00) 2019-01-11 20:14:01
  Ndege nyingine mpya ya Serikali ya Tanzania aina ya Airbus A220-300 iliyopewa jina la Ngorongoro imewasili nchini humo leo na kufanya idadi ya ndege zilizonunuliwa na Serikali kufikia sita.

  Ndege hiyo ambayo tayari ina nakshi za Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) na endapo itakodishwa kwa shirika hilo kama ilivyofanyika kwa ndege nyingine tano itafanya jumla ya ndege za ATCL kufikia 7, ikijumlishwa na ndege yao ya zamani aina ya Bombardier Q300 ambayo sasa ipo katika matengenezo.

  Desemba 23 iliwasili ndege ya kwanza ambayo ilipewa jina la Dodoma. Ndege nyingine zinazomilikiwa na shirika hilo ni Bomberdier Q400-8 tatu na Boeing 87-8 (Dreamliner) moja.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako