• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kamati kuu ya CPC, baraza la serikali ya China na kamati ya kijeshi ya CPC zapongez a mafanikio ya kazi ya chombo cha safari ya anga za juu Chang'e-4

  (GMT+08:00) 2019-01-11 21:03:31

  China imetangaza kuwa kazi ya chombo cha safari ya anga za juu cha nchi hiyo Chang'e-4 ya kupiga picha kwenye sayari ya mwezi imefanyika kwa mafanikio.

  Mjumbe wa ofisi ya siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China CPC, ambaye pia ni naibu waziri mkuu wa China Bw. Liu He, mjumbe wa ofisi ya siasa ya kamati kuu ya CPC, ambaye pia ni naibu mwenyekiti wa kamati ya kijeshi ya CPC Bw. Zhang Youxia wamefuatilia moja kwa moja hali ilivyo katika kituo cha udhibiti cha safari ya anga ya juu cha Beijing.

  Bw. Liu He amesoma barua ya pongezi ya kamati kuu ya CPC, baraza la serikali ya China na kamati ya kijeshi ya kamati kuu ya CPC ambayo imesema, mafanikio ya Chang'e-4 yanaonyesha kufungua kwa pande zote kipindi cha nne cha uchunguzi wa sayari ya mwezi na uchunguzi wa safari ya anga ya juu. Kazi katika siku za usoni zitakuwa ngumu zaidi, na changamoto zitakuwa kubwa zaidi. Amesema anatumai watu wote wa sekta ya safari ya anga ya juu wataendelea kufanya juhudi kwa ajili ya kutimiza ustawi wa China na kutoa mchango zaidi kwa ajili ya kuhimiza ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye mustakbali wa pamoja.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako