• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mkutano ujao wa AU kuangazia hali ya wakimbizi wa Afrika na wakimbizi wa ndani

  (GMT+08:00) 2019-01-12 16:31:51

  Kamati ya Umoja wa Afrika jana ilieleza kuwa Mkutano wa Viongozi wa Afrika utakaofanyika mwezi ujao utaangazia zaidi hali ya wakimbizi wa Afrika, wakimbizi waliorejea makwao, na wakimbizi wa ndani.

  Kupitia taarifa yake AU imesema, Mkutano wa Kamati ya Wawakilishi wa Kudumu wa Umoja wa Afrika unachotarajiwa kufanyika tarehe 15 na 16 huko Addis Ababa, Ethiopia, utakuwa chini ya kauli mbiu ya "Wakimbizi, Waliorejea makwao na Wakimbizi wa ndani: Kuelekea Ufumbuzi wa Kudumu wa Kuwalazimisha Wakimbizi katika Afrika,".

  Mkutano huo unatarajiwa kuwaleta pamoja maofisa wa AU na ujumbe kutoka nchi wanachama 55 wa Umoja wa Afrika na pia kuandaa ajenda ya mkutano wa kilele wa viongozi, ikiwa ni pamoja na mapendekezo yanayofaa kujadiliwa ili baadaye kuzingatiwa na Baraza la Utendaji, ambalo litawaleta pamoja mawaziri wa mambo ya nje wa nchi wanachama wa AU.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako