• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waandishi wa habari wa nchi za Ukanda Mmoja na Njia Moja wasifu mafanikio ya mapambano dhidi ya ugaidi nchini China

    (GMT+08:00) 2019-01-12 16:42:31

    Waandishi wa habari kutoka vyombo vya habari vya nchi sita za Ukanda Mmoja na Njia Moja ziwemo Uturuki, Misri, Afghanistan, Pakistan, Bangladesh na Sri Lanka hivi karibuni walitembelea Maonesho ya mapambano dhidi ya ugaidi ya Mkoa unaojiendesha wa wauigur wa Xinjiang, na kusema ugaidi ni adui wa pamoja wa binadamu, na nchi mbalimbali zinapaswa kushirikiana na kukabiliana na ugaidi kwa pamoja. Vilevile walisifu mafanikio ya serikali ya China katika mapambano dhidi ya ugaidi.

    Mwandishi wa habari kutoka Uturuki Bw. Enes Taha Ersen alisema, serikali ya China imechukua hatua mfululizo zenye ufanisi, na katika miezi 25 iliyopita hayakutokea matukio ya kigaidi mkoani Xinjiang. Aliutakia mkoa wa Xinjiang uwe na utulivu na amani kwa muda mrefu.

    Naye Mhariri wa gezeti la Al-Ahram Ektassdy la Misri Bi. Samia Fakhry Mansour alisema, utulivu ni msingi wa maendeleo, na kuutakia mkoa wa Xinjiang uwe na mustakabali mzuri.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako