• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Usitishwaji wa huduma za serikali nchini Marekani waingia siku ya 22 na kuvunja rikodi

  (GMT+08:00) 2019-01-12 16:51:03

  Usitishwaji wa huduma za serikali kutokana na mzozo kati ya bunge la chini na rais Donald Trump wa Marekani, ambao wanakataa kutoa fedha kwa ajili ya kujengwa ukuta wa mpakani leo unaingia siku ya 22, ikiwa umechukua muda mrefu zaidi katika historia ya Marekani.

  Hadi sasa hakuna maelewano, wala makubaliano, na hakuna njia nyingine iliyo rahisi. Rais Trump ameapa kupiga kura ya turufu kwa mswada wowote wa matumizi ambao hautakuwa na dola bilioni 5.7 anazohitaji za ukuta kwenye mpaka kati ya Marekani na Mexico, wakati ambapo wabunge wa Democratic nao wakiapa kuzuia matumizi yoyote yatakayokuwa na pesa za ukuta. Hakuna hata upande mmoja unaoonekana kurudi nyuma.

  Hata hivyo jana rais Trump hakuonesha dalili ya kutangaza haraka hali ya dharura ili kutumia jeshi kujenga ukuta, hatua ambayo inaweza kumaliza kizuizi lakini inatarajiwa kusababisha mapambano makali ya kisheria.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako