• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kukabidhi madaraka kwa amani kunaendana na maslahi ya wananchi wa DRC

  (GMT+08:00) 2019-01-12 17:25:05

  Mjumbe wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Bw. Ma Zhaoxu jana alisema, kukabidhi madaraka kwa amani kunaendana na maslahi ya wananchi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, na China inatumai pande mbalimbali za DRC zitajizuia, kutatua mgogoro kwa mazungumzo na kulinda amani na utulivu wa taifa.

  Bw. Ma amesema, China siku zote inaunga mkono mchakato wa amani wa DRC, kushiriki operesheni ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa nchini DRC, na itaendelea kutoa msaada wa kibinadamu nchini DRC, kushiriki kwenye ujenzi wa maendeleo ya uchumi na jamii, ili kutoa mchango kwa ajili ya amani, utulivu na maendeleo ya nchi hiyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako