• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuinua kiwango cha huduma za matibabu kwenye maeneo maskini

    (GMT+08:00) 2019-01-13 20:25:02

    Kamati ya afya ya taifa la China hivi karibuni imetangaza kuwa, China itainua kiwango cha huduma za matibabu kwenye maeneo yenye watu maskini, ili kuhakikisha hospitali za ngazi mbalimbali za wilaya, tarafa na vijiji, zinafikia vigezo vilivyowekwa kabla ya mwaka 2020.

    Msemaji wa kamati hiyo Bw. Hu Qiangqiang alisema, hospitali zenye kiwango cha juu zitatoa mafunzo kwa madaktari wa hospitali za wilaya maskini, na kila hospitali ya tarafa itakuwa na mtaalamu mmoja kabla ya mwaka 2020.

    Msemaji huyo pia amesema huduma za matibabu kwa njia ya mtandao zitafikia hospitali zote za tarafa maskini, na madaktari wanaohudumia hospitali za chini watapata tuzo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako