• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Kombe la Mapinduzi, Azam FC yaendeleza ubabe, yachukua Ubingwa

    (GMT+08:00) 2019-01-14 08:48:00
    Mashabiki wa soka nchini Tanzania mwishoni mwa wiki wameshuhudia burudani kadhaa za soka,michuano ya Kombe la Mapinduzi imefikia tamati jana kwa kuwakutanisha vigogo wa soka Tanzania Bara, Simba Sports Club na Azam FC.

    Azam FC wameendeleza ubabe na kunyakua ubingwa wa Muungano mara tatu mfululizo na hivyo kuchukua kombe hilo moja kwa moja.

    Mchezo wa jana ulikuwa mkali licha ya Simba kutumia kikosi chake cha pili, hadi kipenga cha mwisho, Azam wametoka kifua mbele kwa ushindi wa magoli 2-1.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako