• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Thamani ya biashara ya njeya China kwa mwaka jana yafikia yuan trilioni 30

    (GMT+08:00) 2019-01-14 10:31:38

    Takwimu zilizotolewa leo na idara kuu ya forodha ya China zinaonyesha kuwa, mwaka jana thamani ya biashara kati ya China na nchi za nje imefikia kiwango cha juu katika historia, ambayo imefikia yuan trilioni 30.51, ambayo ni sawa na dola za kimarekani trilioni 4.5, ikiwa ni ongezeko la asilimia 9.7 kuliko mwaka 2017.

    Takwimu zinaonyesha kuwa thamani ya uuzaji bidhaa nje imefikia yuan trilioni 16.42, likiwa ni ongezeko la asilimia 7.1, thamani ya uagizaji bidhaa kutoka nje imefikia yuan trilioni 14.09, ambayo ni ongezeko la asilimia 12.9.

    Takwimu pia zinaonyesha kuwa, nguvu ya ushirikiano wa kibiashara kati ya China na nchi za "Ukanda Mmoja na Njia Moja" iliendelea kuonekana katika mwaka 2018, na thamani ya biashara kati ya China na nchi hizo imeongezeka kwa asilimia 13.3.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako