Waziri Mkuu wa Uingereza Bibi Theresa May amesema atatoa hotuba ya mwisho kwenye mijadala kuhusu hatma ya Uingereza kwenye Umoja wa Ulaya.
Licha ya kuwataka wabunge kuunga mkono makubaliano aliyofikia na Umoja wa Ulaya, ni wachache wanaoona kuwa Bibi May ana uungaji mkono wa kutosha kati ya wabunge 640 wanaopiga kura leo jioni. Akishindwa kwenye upigaji kura huo kama inavyotarajiwa na wengi, Bibi May atatakiwa kuja na mpango mpya bungeni jumatatu ijayo.
Kiongozi wa chama cha Labour Bw. Jeremy Corbyn amekutana na wabunge wa chama chake na kuwaambia kuwa kutakuwa na upigaji kura wa kutokuwa na imani na Bibi May.
Wakati huo huo kiongozi wa walio wengi bungeni Bw Gareth Johnson, jana alijuzulu nafasi yake siku moja kabla ya kupiga kura. Mhafidhina huyo ameonya kuwa kama makubaliano ya Bibi May yakikataliwa huenda Uingereza isijitoe Umoja wa Ulaya.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |