• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Thamani ya uwekezaji wa kigeni nchini China mwaka 2018 yafikia kiwango cha juu katika historia

    (GMT+08:00) 2019-01-15 18:16:29

    Takwimu zilizotolewa na wizara ya biashara ya China zinaonesha kuwa, thamani ya uwekezaji wa kigeni nchini China kwa mwaka 2018 China ilifikia dola za kimarekani bilioni 134.9, na kuongezeka kwa asilimia 3 kuliko mwaka 2017.

    Takwimu hizo zimeonyesha kuwa, mwezi Desemba mwaka 2018 uwekezaji wa kigeni nchini China ulifikia dola za kimarekani bilioni 13.97, na kuongezeka asilimia 23.2 kuliko mwaka 2017 wakati kama huo.

    Mkurugenzi wa idara ya uwekezaji wa nje iliyo chini ya wizara ya biashara ya China Bw. Tang Wenhong amesema, matumizi halisi ya uwekezaji wa nje kwenye sekta ya viwanda umeongezeka kwa kasi nchini China. Ameongeza kuwa kuanzia mwezi Januari hadi Desemba mwaka 2018 uwekezaji wa nje uliotumika kwenye sekta ya viwanda umeongezeka kwa asilimia 20.1, na kuchukua asilimia 30.6 kwenye uwekezaji wa nje uliotumika mwaka 2018 nchini China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako