• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yafanya juhudi za kuhimiza matumizi ya fedha, kutuliza biashara ya nje na uwekezaji kutoka nje

    (GMT+08:00) 2019-01-15 19:14:44

    Waziri wa biashara wa China Bw. Zhong Shan hivi karibuni alisema, Mwaka 2019 wizara hiyo itafanya juhudi za kuhimiza matumizi ya fedha, kutuliza biashara ya nje na uwekezaji kutoka nje; kufanya maandalizi mazuri kwa ajili ya Maonesho ya pili ya uagizaji na uuzaji wa bidhaa nje ya China, kukabiliana ipasavyo na mgogoro wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Marekani, na kusukuma mbele ujenzi wa maeneo ya majaribio ya biashara huria, pamoja na bandari ya biashara huria.

    Mwaka 2018 matumizi ya fedha nchini China yanatazamiwa kuzidi dola za kimarekani trilioni 5.6, likiwa ni ongezeko la asilimia 9.1, na kuwa msukumo mkubwa wa ongezeko la uchumi katika miaka mitano iliyopita, hali ambayo pia imeonesha kuwa China inapiga hatua thabiti katika mwelekeo wa kuwa nchi kubwa ya matumizi ya fedha inayoongoza duniani. Waziri wa biashara wa China Bw. Zhong Shan anasema:

    "Tutachukua hatua tatu ili kuhimiza matumizi ya fedha, nazo ni pamoja na kuongeza matumizi ya fedha mijini, kuhimiza matumizi ya fedha vijijini, na kuendeleza matumizi ya fedha katika sekta ya utoaji wa huduma."

    akitupia macho siku za baadaye Bw. Zhong Shan anasema, China bado ni nchi inayovutia kwa wingi zaidi uwekezaji kutoka nje duniani, Benki ya Dunia imepandisha nafasi yake kwa 32 kuhusu mazingira ya uendeshaji wa biashara. Takwimu zilizotolewa mwezi uliopita na Kamati ya biashara kati ya Marekani na China zimeonesha kuwa, asilimia 90 ya viwanda vinaona kuwa China ni moja kati ya masoko muhimu zaidi duniani, zaidi ya asilimia 95 ya viwanda vitaongeza au kudumisha kiwango cha uwekezaji nchini China katika mwaka mmoja ujao. Pia amedokeza kuwa wizara hiyo itaendelea kutekeleza mipango ya kuhimiza uwekezaji kutoka nje. Anasema:

    "Hatua za kutuliza uwekezaji kutoka nje ni pamoja na kupanua maeneo ya ufunguaji mlango, kuongeza nguvu katika kuvutia uwekezaji, pamoja na kujenga uwanda mpya wa juu wa ufunguaji mlango ikiwa ni pamoja na kupanua eneo la majaribio la biashara huria mjini Shanghai, na kufanya utafiti kuhusu kujenga bandari ya biashara huria mkoani Hainan."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako