• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • RIADHA: Rutto na Kitur kushiriki mbio za Mumbai

    (GMT+08:00) 2019-01-16 08:36:15
    Mabingwa wa riadha za Mumbai, wakenya Evans Rutto wa mwaka 2014 na Bornes Kitur wa mwaka 2017 wako katika orodha ya wakimbiaji 46,000 watakaoshiriki makala ya 16 ya mbio hizi za kimataifa nchini India zitakazofanyika Januari 20 mwaka huu.

    Wapinzani wa Rutto ni wakali toka Ethiopia Solomon Deksisa ambaye ni bingwa mtetezi, Chele Dechasa na Abraham Girma.

    Kutoka orodha ya 46, 000 ni 8, 414 pekee ndio watashindana katika mbio za kilomita 42, huku waliosalia wakitimka katika mbio za kilomita 21 na kilomita 10.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako