Wito huo wa ADAK umetolewa siku chache baada ya rais wa shirikisho la riadha la Kenya (AK) Jackson Tuwei kuwasihi wanariadha kuachana na njia ya mkato ya kupata ufanisi ili kusafisha jina la nchi hiyo.
Kwa masikitiko ameeleza kuwa Kenya inaelekea kupigwa marufuku na shirikisho la riadha duniani (IAAF) kutokana na watumiaji wa dawa hizo haramu mashindanoni kuongezeka.
Mbali na Kenya, nchi zingine zinazotupiwa macho na IAAF ni Ethiopia, Belarus, India na Ukraine.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |