• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Ligi kuu Tanzania Bara: Yanga yaifanyia kitu mbaya Mwadui

    (GMT+08:00) 2019-01-16 08:38:14
    Mabao ya Ibrahim Ajib na Amis Tambwe yamewatanguliza kifua mbele Yanga katika dakika 45 za kpindi cha kwanza katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara (TPL) uliopigwa jana uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

    Vinara hao wa ligi hiyo wameendelea kuweka rekodi ya kutofungwa baada ya mchezo wa jana kuibuka na ushindi wa magoli 3-1 na kuwaacha watani wake wa jadi Simba Sports Club kwa alama 20.

    Ushindi huo unaifanya timu hiyo ya wananchi kufikisha alama 53 baada ya kucheza mechi 19. Tofauti ya alama hizo kati ya Yanga na Simba itawalazimu mabingwa watetezi Simba wenye viporo saba kushinda mechi zote huku ikiwaombea watani wao wapoteze ili kuweza kuwafikia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako