• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mahakama ya Russia yaongeza muda wa kushikiliwa kwa wanamaji wa Ukraine

    (GMT+08:00) 2019-01-16 09:03:06

    Mahakama moja mjini Moscow imeongeza muda wa kushikiliwa kwa wanamaji 12 wa Ukraine wanaotuhumiwa kuvuka kiharamu mpaka wa Russia katika Mlango wa Bahari wa Kerch hadi tarehe 24, Aprili. Wanamaji hao wanasubiri kupelekwa mahakamani ili kesi zao zisikilizwe. Tarehe 25, Novemba mwaka jana, Russia ilikamata meli tatu za jeshi la majini la Ukraine na wanamaji 24 waliokuwa kwenye meli wakijaribu kupita kwenye Mlango wa Bahari wa Kerch kutoka Bahari Nyeusi na kwenda Bahari ya Azov.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako