• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 15 wahofiwa kuuawa kwenye shambulizi la kigaidi Nairobi

    (GMT+08:00) 2019-01-16 10:38:40

    Karibu watu 15 wanahofiwa kuuawa nchini Kenya kwenye shambulizi la kigaidi katika hoteli ya Dusit iliyoko kwenye eneo la Westlands mjini Nairobi.

    Watu wanaoshukiwa kuwa magaidi wamevamia hoteli hii ya Dust na kuanza kuwamiminia watu risasi. Hadi wakati wa kwenda hewani maofisa wa polisi walikuwa bado wanapambana na magaidi hao. Akizungumza na wanahabari Inpekta mkuu wa polisi Joseph Boinett amesema vikosi vya usalama vinaendelea kupambana na magaidi hao.  Anasema, "Mwendo wa saa tisa alasiri kundi la watu waliokuwa wamejihami walishambulia hoteli ya Dusit ikiwa ni shambulio tunaloshuku kuwa la kigaidi. Bado majambazi hao wako kwenye Jengo la hoteli lakini maofisa wetu wanapambana nao vilivyo. Tumeokoa watu wengi kwa kuwaondoa kwenye hoteli hiyo'

    Shambulizi hili linakuja miaka michache tu baada ya shambulizi la Westgate ambalo lilisababisha vifo vya watu wengi na kuwaacha wengine wengi na majeraha.

    Kundi la kigaidi la Al-shabab tayari limekiri kuhusika na shambulizi hili.

    Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Bw. Antonio Gutteres amelaani shambulizi hilo, na kusema anafuatilia kwa karibu maendeleo ya tukio hilo. Mwenyekiti wa baraza la Umoja wa mataifa Bibi Maria Fernanda Espinosa pia amelaani shambulizi hilo, na kusema hakuna kisingizio cha kutumia ugaidi na mabavu dhidi ya watu wasio na hatia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako