• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sherehe ya kukabidhi uenyekiti wa Kundi la nchi 77 na China yafanyika

    (GMT+08:00) 2019-01-16 18:10:47

    Sherehe ya kukabidhi uenyekiti wa Kundi la nchi 77 na China imefanyika jana kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, na Palestina imekuwa mwenyekiti wa "Kundi la nchi 77 na China" mwaka 2019.

    Sherehe hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Rais Mahmoud Abbas wa Palestina, waziri wa mambo ya nje wa Misri Bw. Sameh Hassan Shoukry, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres, na balozi wa China kwenye Umoja huo Bw. Ma Zhaoxu. Washiriki wapato 200 wamesifu umuhimu uliooneshwa na "Kundi la nchi 77 na China" katika kuhimiza utekelezaji wa ajenda za maendeleo endelevu mwaka 2030 na kukabiliana na changamoto zinazotokana na mabadiliko ya hali ya hewa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako