• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa Russia asema mwelekeo wa kupunguza utegemezi kwa dola ya Marekani duniani utaimarika

    (GMT+08:00) 2019-01-16 18:31:59

    Waziri mkuu wa Russia Bw. Dimitri Medvedev huko Moscow amesema mwelekeo wa kupunguza utegemezi wa uchumi kwa dola za Marekani duniani utaimarika.

    Akizungumza kwenye mkutano wa baraza la Gaidar, Bw. Medvedev amesema hivi sasa nchi kadhaa zinatarajia kupunguza utegemezi wa dola ya kimarekani kwa uchumi wao, na hali hiyo itaimarika katika siku za baadaye.

    Bw. Medvedev amesema, dola ya kimarekani ni sarafu kuu ya akiba duniani, lakini Marekani inaendelea kuondoa imani ya dunia katika dola yake na kuchochea mchakato wa kuondoa dola za kimarekani.

    Ameongeza kuwa, Marekani inajaribu kuhamisha tishio la ndani la kiuchumi na kisiasa kwa pande nyingine shiriki za uchumi wa dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako