• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ligi ya Mabingwa Afrika: Simba SC kuondoka leo kuwafuata AS Vita DRC na jeshi la wachezaji 20

    (GMT+08:00) 2019-01-17 08:53:30
    Nahonda wa klabu ya Simba ya Tanzania John Bocco hatasafiri na timu timu yake leo kwenda Kinshasa DRC kwa ajili ya mchezo wa kundi D ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji AS Vita mchezo utakaopigwa Jumamosi hii.

    Daktari wa klabu hiyo Yassin Gembe amewaambia waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam kuwa Bocco atakuwa nje ya uwanja kwa siku 10 baada ya kuumia kwenye mchezo wa klabu hiyo na JS Saoura ya Algeria uliopigwa uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

    AS Vita ilipoteza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Al Ahly ya Misri katika uwanja wa Borg El Arab mjini Alexandria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako