• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda mwenyeji michezo ya vijana ya Olimpiki (ANOCA)

    (GMT+08:00) 2019-01-17 08:53:59

    Rwanda mwaka huu inatarajiwa kuwa mwenyeji wa michezo ya Olimpiki kwa vijana ya Afrika (ANOCA). Kwa mujibu wa rais wa kamati ya michezo ya olimpiki nchini humo bwana Valens Munyabagisha amesema michuano hiyo ya siku tano itaanza April 2 hadi 6 mwaka huu mjini Huye Rwanda.

    Michezo itakayochezwa kwenye michuano hiyo ni pamoja na Mbio za baiskeli, taekwondo, kikapu, riadha na voleboli ya ufukweni, huku nchi 11 zitashiriki ambazo ni Tanzania, Sudan, Burundi, Ethiopia, Misri, Eritrea, Kenya, Sudan Kusini, Uganda, Somalia na mwenyeji Rwanda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako