• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Hatimaye Mieno atua St. George Ethiopia, Ndemla na Chambo majaribio Sweden

    (GMT+08:00) 2019-01-17 08:54:57
    Kiungo wa Gor Mahia Humphrey Mieno hatimaye amejiunga rasmi na vigogo wa soka wan chi jirani ya Ethiopia, St. George. Mieno ambaye pia aliwahi kusakata kwa mabingwa wa zamani Tusker na Sofapaka, mwanzoni mwa wiki hii alimwaga wino wa mkataba wa miaka miwili baada ya maafisa wa K'Ogalo na wenzao wa St Georges kuafikiana wakiwa wameshiriki mwezi moja wa majadiliano ya kina.

    Mwanasoka huyo sasa atajiunga na golikipa mahiri wa timu ya taifa Harambee Stars Patrick Matasi anayedakia timu hiyo na kocha wa zamani wa Sofapaka Steward Hall ambaye pia alikuwa mkufunzi wa Mieno alipochezea Batoto ba Mungu.

    Kwingineko kiungo chipukizi wa Tanzania Said Hamis Ndemla leo anatarajiwa kuanza majaribio mafupi katika Klabu ya AFC Eskilstuna ya ligi kuu nchini Sweden.

    Hiyo ni baada ya mchezaji huyo wa klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam kuwasili mjini Stockholm aiwa maeongozana na mshambuliaji mwingine chipukizi wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Rashid Chambo wa JKT Ruvu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako