• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la usalama la UM launda tume ya kuunga mkono makubaliano ya Hodeidah, Yemen

    (GMT+08:00) 2019-01-17 09:25:54

    Baraza la usalama la Umoja wa mataifa limepitisha azimio la kuunda tume ya kuunga mkono utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa kati ya serikali ya Yemen na waasi wa Houthi.

    Azimio namna 2452 limeungwa mkono na wajumbe wote 15 wa baraza la usalama, kuanzisha tume hiyo itakayofanya kazi ya awali kwa kipindi cha miezi sita, kuunga mkono makubaliano yaliyofikiwa mjini Stockholm kati ya pande hizo mbili kuhusu mji wa Hodeidah, na bandari za Salif na Ras Issa.

    Hatua hii imekuja baada ya baraza la usalama kutoa idhini kwa kikundi cha utangulizi chenye watu 30 kusimamia na kuunga mkono utekelezaji wa makubaliano hayo.

    Habari pia zinasema msemaji wa umoja wa mataifa Bw. Stephen Dujarric amefahamisha kuwa mazungumzo mengine yameanza mjini Amman Jordan kuhusu mabadilishano ya wafungwa wa vita ya wenyewe kwa wenyewe Yemen.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako