• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wataalamu UM washauri Afrika kuvuna maji ya mvua kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa

    (GMT+08:00) 2019-01-17 09:26:34

    Mtaalamu kutoka Shirika la elimu, sayansi na utamaduni la Umoja wa mataifa UNESCO Bw. Jaykumar Ramasamy amezishauri nchi za Afrika kuvuna maji ya mvua ili kupunguza madhara ya mabadiliko ya hali ya hewa.

    Akuiongea na wanahabari mjini Nairobi Bw. Ramasamy amesema njia moja ya Afrika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa ni kuvuna maji ya mvua, ambayo yatasaidia kuongeza maji ya ardhini yanayotegemewa kuwa chanzo cha maji.

    Bw. Ramasamy amesema UNESCO tayari imefanya upimaji kwenye maeneo yote ya chini ya ardhi, na kusema maji hayo yatakuwa chanzo kikuu cha maji kwenye eneo kubwa la Afrika, hasa maeneo kame na nusu kame, kwa kuwa maji ya juu ya ardhi yanapungua.

    Waziri wa maji wa Kenya Bw. Simon Chelugui amesema asilimia 75 ya watu barani Afrika wanatumia maji ya ardhini kama chanzo kikuu cha maji ya kunywa, kunywesha mifugo na matumizi ya maji mijini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako