• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu zaidi ya 1,600 wafariki katika ajali za barabarani Afrika Kusini katika msimu wa sikukuu

    (GMT+08:00) 2019-01-17 09:45:42

    Jumla ya watu 1,612 wamefariki dunia kwenye ajali za barabarani katika msimu wa sikukuu nchini Afrika Kusini. Ripoti iliyotolewa na waziri wa usafiri wa nchi hiyo Bw. Blade Nzimande, inasema kuanzia tarehe mosi Disemba mwaka jana hadi tarehe 8 Januari mwaka huu, idadi ya vifo vilivyotokana na ajali za barabarani imeongezeka kwa asilimia 5 kuliko mwaka wa 2017 hadi 2018 kipindi kama hicho. Mkoa wa Kwazulu-Natal umeongoza kwa kuwa na vifo 328, ukifuatiwa Cape Mashariki ukiwa na watu 238. Mabasi madogo na malori yalihusishwa katika baadhi ya ajali kubwa na kusababisha vifo vya watu 54.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako