• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Ethiopia yasaini makubaliano na kampuni ya China kuhusu ujenzi wa barabara

    (GMT+08:00) 2019-01-17 09:50:46

    Mamlaka ya barabara ya Ethiopia ERA imesaini makubaliano yenye thamani ya dola milioni 3,300 za kimarekani na kampuni ya Sinohydro ya China kuhusu ujenzi wa barabara.

    Taarifa iliyotolewa jana na ERA inasema, kampuni ya Sinohydro itakarabati upya barabara yenye urefu wa kilomita 80.5 kati ya Gedo na Menabegna kutoka kiwango cha changarawe hadi kiwango cha lami, na fedha za mradi huu zitatolewa na Benki ya Maendeleo ya Afrika na vyanzo kutoka Mashariki ya Kati.

    Serikali ya Ethiopia inalenga kuongeza urefu wa barabara kuu nchini humo kutoka kilomita laki moja za mwaka 2015 hadi laki mbili mwaka 2020.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako