• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nchi za Afrika zaahidi kuondoa sintofahamu zinazowakabili wakimbizi wa ndani na nje

    (GMT+08:00) 2019-01-17 09:51:09

    Nchi za Afrika zimeahidi kuondoa sintofahamu zinazowakabili wakimbizi barani Afrika.

    Wajumbe wa nchi wanachama 55 wa Umoja wa Afrika wametoa ahadi hiyo kwenye mkutano wa 37 wa kamati ya wajumbe wa Umoja wa Afrika uliofanyika kuanzia tarehe 15 hadi 16 mjini Addis Ababa. Mkutano huo umefuatilia hali ya wakimbizi wa ndani na nje.

    Naibu mwenyekiti wa halmashauri kuu ya Umoja wa Afrika Bw. Kwesi Quartey, amesema kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe na migogoro mingine ya ndani, waafrika wengi wamepoteza makazi na baadhi yao wamekimbilia sehemu nyingine kutafuta riziki. Amesema mwaka huu Umoja wa Afrika utafuatilia zaidi suala la watu wasio na uraia na makazi, suala hilo linahusiana na utawala bora, haki za binadamu na demokrasia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako