• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa laeleza wasiwasi wake kuhusu hali ya usalama nchini Mali

    (GMT+08:00) 2019-01-17 16:15:41

    Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeeleza wasiwasi wake kuhusu kuendelea kuzorota kwa hali ya usalama nchini Mali, na kuitaka serikali na makundi yenye silaha kutekeleza makubaliano ya Amani yaliyofikiwa mwaka 2015.

    Wajumbe wa Baraza hilo wamelaani vikali mashambulizi yanayoendelea, ikiwemo mashambulizi ya kigaidi dhidi ya raia, wawakilishi kutoka mashirika ya ndani, ya kikanda na ya taifa, na pia vikosi vya usalama vya Umoja wa Mataifa, vya kimataifa pamoja na vya ndani ya Mali.

    Pia wajumbe hao wamelaani kuibuka kwa vurugu kati ya makabila ambayo imesababisha vifo vya raia wasio na hatia, na kuitaka serikali ya Mali kuhakikisha kuwa watu wanaohusika na uhalifu unaohusiana na ukiukwaji wa haki za binadamu na sheria za kimataifa za kibinadamu wanachukuliwa hatua na kufikishwa mbele ya sheria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako