• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matumaini ya kampuni za Marekani kuhusu mustakabali wa uchumi yapungua

    (GMT+08:00) 2019-01-17 17:07:46

    Ripoti ya uchunguzi wa hali ya uchumi nchini Marekani iliyotolewa jana na kamati ya Benki Kuu ya nchi hiyo FED inaonesha kuwa, kuanzia mwanzo wa mwezi Desemba mwaka jana hadi mwezi Januari mwaka huu, uchumi wa Marekani umeongezeka kwa utulivu, lakini matumaini ya kampuni za Marekani kuhusu mustakabali wa uchumi yamepungua.

    Ripoti hiyo imesema, kwa ujumla mustakabali wa uchumi wa Marekani ni mzuri, lakini kutokana na kuongezeka wa mabadiliko ya soko la fedha, kupanda kwa riba ya muda mfupi, kushuka kwa bei ya nishati na kuongezeka kwa wasiwasi wa kibiashara na siasa, kampuni za Marekani zimepunguza matumaini yao kuhusu mustakabali wa nchi hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako