• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa Israel kufanya ziara nchini Chad kwa ajili ya mazungumzo ya kurejesha uhusiano wa kidiplomasia

    (GMT+08:00) 2019-01-17 18:42:30

    Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu atafanya ziara nchini Chad tarehe 20 mwezi huu, ambapo anatarajiwa kutangaza kurejea kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya Israel na Chad.

    Taarifa iliyotolewa na ofisi ya waziri mkuu huyo imesema, ziara hiyo inafuata ziara ya siku mbili iliyofanywa na rais Idriss Derby wa Chad nchini Israel mwezi Novemba mwaka jana, ambapo viongozi hao walikutana na kujadili vita dhidi ya ugaidi na ushirikiano wa pande mbili katika nyanja za kilimo, umeme wa jua na maji.

    Chad, ambayo ni nchi yenye idadi kubwa ya waislam katikati ya Afrika, ilivunja uhusiano wa kidiplomasia na Israel mwaka 1972.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako