• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatumai Marekani kuchukua uhusiano kati ya pande hizo kwa msimamo wa kimantiki

    (GMT+08:00) 2019-01-17 18:48:07

    Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya China Bi. Hua Chunying amesema China inatumai kuwa Marekani itachukua msimamo wa kimantiki kwa maendeleo ya China na uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

    Bi. Hua pia ameitaka Marekani kuacha kuingilia kati mambo ya ndani ya China na kuharibu maslahi ya China katika masuala husika, na kujishughulisha zaidi na mambo yanayoongeza uaminifu na ushirikiano kati ya pande hizo. Amesema Marekani inatakiwa kushirikiana na China katika kulinda uhusiano kati ya pande hizo ili kupata maendeleo mazuri kwa hatua madhubuti.

    Wakati huohuo, waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi alipohojiwa na Gazeti la Renminribao ameeleza kuwa, maslahi ya pamoja kati ya pande hizo ni mengi kuliko tofauti zilizopo, na haipaswi kutambua uhusiano kati ya pande hizo kutokana na migogoro kati yao, wala haipaswi kuamua uhusiano huo kwa njia zisizo sahihi.

    Huu ni mwaka wa 40 tangu China na Marekani zianzishe uhusiano wa kibalozi kati yao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako