• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wakulima wa miwa kusubiri zaidi baada ya vikao vya kutafuta mabadiliko kusitishwa

  (GMT+08:00) 2019-01-17 18:59:22

  Wakulima wa miwa nchini Kenya watalazimika kusubiri kwa muda zaidi ili kuona mabadiliko yaliyoamriwa na rais Uhuru Kenyatta kutekelezwa. Jopo linaloongozwa na Gavana wa Kakamega Wycliffe Oparanya limefuta vikao vyake vya kuwashirikisha wananchi baada ya kundi la wakulima wa miwa kutishia kufanya vikao vyake kutokana na kucheleweshwa kwa malipo. Vikao vya kuwashirikisha wananchi vilitakiwa kudumu kwa siku nne. Mwaka jana, rais Uhuru Kenyatta aliamrisha wizara ya kilimo kuangalia upya bei ya sukari, uagizwaji wa sukari kutoka nje na muundo wa ulipaji kodi ili kutafuta mwelekeo wa kutatua matatizo yanayoikumba sekta ya sukari Kenya

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako