• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • TADB yatakiwa kubadili mfumo wa malipo

  (GMT+08:00) 2019-01-17 18:59:40

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameiagiza Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kubadilisha mfumo wake wa malipo ili iweze kuharakisha malipo kwa wakulima wa korosho ambao wameshahakikiwa.

  Alisema ametoa agizo hilo baada ya Serikali kuendelea kupokea malalamiko kutoka kwa wakulima kuhusu suala la malipo wakati kwa kawaida malipo ya mkupuo hukamilika ifikapo Januari 10 ya kila mwaka.

  Alitoa agizo hilo wakati akizungumza na wakuu wa mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma pamoja na mkurugenzi mkuu wa TADB, Japhet Justine kwenye kikao alichokiendesha kwa njia ya video kutoka ofisini kwake mjini Dodoma.

  Waziri Mkuu pia alihoji sababu za benki hiyo kutoshirikiana na vyama vikuu au vyama vya msingi ili kubaini idadi halisi ya wakulima na idadi kamili ya kiasi walichovuna kwa sababu kila chama cha msingi kina wanachama wanaojulikana.

  Waziri Mkuu pia aliwataka wakuu wa mikoa hiyo wahuishe taarifa zao na wamtumie ili aweze kuzitumia kuratibu zoezi zima na kwamba amefanya mazungumzo na wakurugenzi wa benki za CRDB na NMB na kuwasisitiza kuwa suala la miamala ya malipo ya korosho lifanywe mchana na usiku ili malipo yakamilike kabla ya Januari mwishoni .

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako