• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yawafutia makosa wafanyabishara wasiokuwa na leseni

    (GMT+08:00) 2019-01-17 19:00:15

    Serikali ya Tanzania imeamua kuwafutia makosa wote walioshtakiwa kwa kutokuwa na leseni, ikitaka waachiwe huru. Tangazo hilo la serikali linakuja siku moja tu baada ya wavuvi na wauzaji wa sakama katika Soko la Kimataifa la Samaki la Feri kurushia lawama Serikali kutokana na kuadimika kwa kitoweo hicho,

    Jana, wavuvi na wauza samaki walisema Serikali inahusika na kuadimika kwa samaki katika soko hilo baada ya kuanzisha operesheni ya ukaguzi wa leseni za uvuvi, ikiwa ni tofauti na maelezo yaliyotolewa kwa maandishi na Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

    Mwenyekiti wa Umoja wa Madalali wa Biashara ya Samaki, Abdallah Hamis alisema uvuvi umeshuka kwa asilimia 70 na kuathiri upatikanaji wa samaki aina ya vibua ambao wamepanda kutoka wastani wa Sh75,000 kwa kilo 25 hadi Sh150,000.

    Hata hivyo, wakati taarifa zikionyesha kupanda ghafla kwa bei ya samaki, Serikali imewafutia adhabu wavuvi wote waliokamatwa mwaka huu kwa makosa ya kutokuwa na leseni na kuwataka wanaowashikilia, wawaachie mara moja. Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega alisema licha ya uamuzi huo tangu juzi wavuvi hawajafanya kazi yao kutokana na baadhi yao kukamatwa.

    Aliagiza wavuvi wote waendelee kukatiwa leseni hadi Januari 31, na kuwataka maofisa wa wizara na halmashauri waanze kuwafuata kwenye mialo ili kuwakatia leseni kwa mujibu wa sheria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako