• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yasema wote waliopotea baada ya shambulizi la kigaidi wamepatikana

    (GMT+08:00) 2019-01-18 08:40:37

    Shirika la msalaba mwekundu la Kenya KRCS limesema watu 94 walioripotiwa kutojulikana walipo baada ya kutokea kwa shambulizi la kigaidi dhidi ya hoteli moja kwenye wilaya ya Westlands mjini Nairobi, wamepatikana.

    Shirika hilo limesema watu hao 94 wote walipatikana jana, na sasa limeanza kuwapa ushauri nasaha walionusurika na familia za wahanga 21 waliouawa katika shambulizi hilo.

    Hatua hiyo imekuja baada ya polisi nchini Kenya kutangaza kuwa shambulizi hilo lililotokea kwenye eneo la Riverside Drive limesababisha vifo vya watu 21 na wengine wengi kujeruhiwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako