• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Klabu Bingwa Afrika: Balozi aipokea Simba SC DRC

    (GMT+08:00) 2019-01-18 08:50:15
    Msafara wa wachezaji 20 wa klabu ya Simba ya Tanzania umewasilia salama mjini Kinshasa DRC kwa ajili ya mchezo wa klabu bingwa Afrika hatua ya makundi dhidi ya AS Vita ya nchini humo.

    Msafara huo umepokelewa na Balozi wa Tanzania nchini humo Luteni Jenerali mstaafu Paul Ignac Mella.

    Balozi Mella amewatoa hofu viongozi na wachezaji wa Simba kuwa hali ya Kinshasa ni salama na hakuna vita wala hakutegemei kuwepo kwa vita.

    Simba itakutana na AS Vita kesho Jumamosi, huku Simba ikiongoza kundi D kwa kuwa na Pointi tatu na magoli matatu ya kuifunga huku AS Vita haijapata pointi baada ya kukubali kipigo toka kwa Al Ahly ya Misri hivyo kukamata nafasi ya tatu katika msimamo wa kundi hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako