• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Mwandishi wa habari aliyefichua mwamuzi kupokea rushwa auawa

    (GMT+08:00) 2019-01-18 08:52:02
    Moja kati ya habari ya kuhuzunisha katika tasnia ya michezo ni kuuawa kwa mwandishi wa habari za uchunguzi Ahmed Hussein-Suale kwa kupigwa risasi tatu na watu wasiojulikana wakati akitoka katika mizunguko yake akirudi nyumbani kwake mjini Madina Accra Ghana.

    Mauaji ya kikatili kwa mwandishi huyo aliyevumbua skendo ya rushwa kwa aliyekuwa raisi wa shirikisho la soka Ghana bwana Akwesi Nyantakyo na kusababisha raisi huyo wa soka nchini Ghana kufungiwa maisha kutojihusisha na masuala ya michezo.

    Mwandishi huyo alijizolea umaarufu nchini Ghana na Afrika kwa ujumla, kutokana na kufichua siri nyingi juu ya kukithiri kwa rushwa kwenye soka barani Afrika, ikiwemo ya mwamuzi wa Kenya aliyeondolewa katika waamuzi waliokuwa wamepangwa kuchezesha Kombe la Dunia mwaka 2018 baada ya uchunguzi wake kumbaini kwamba alipokea rushwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako