• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mjumbe maalumu wa rais wa China akutana na rais wa Guinea ya Ikweta

    (GMT+08:00) 2019-01-18 09:10:53

    Mjumbe maalumu wa rais wa China Bw Yang Jiechi jana alikutana na rais Teodoro Obiang Nguema Mabasogo wa Guinea ya Ikweta mjini Malabo.

    Bw Yang amekabidhi salamu za rais Xi Jinping kwa rais Nguema, na kusema katika mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano wa China na Afrika FOCAC uliofanyika mwaka jana mjini Beijing, marais wa nchi hizo mbili walikutana na kufikia makubaliano juu ya kuendeleza uhusiano wa pande mbili. Amesema China inapenda kuhimiza ujenzi wa "Ukanda mmoja, njia moja", kutekeleza "hatua kuu nane", ili kuimarisha ushirikiano wa kiutendaji, na kuwanufaisha wananchi wake.

    Rais Nguema amesema China ni mwenzi muhimu wa ushirikiano kwa nchi yake, na inakaribisha makampuni ya China kuwekeza nchini humo, na kuimarisha zaidi ushirikiano wa kunufaishana na China. Pia amesema Guinea ya Ikweta itaendelea kuimarisha mawasiliano na uratibu na China katika mambo ya kikanda na kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako